• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njia mpya za safari za ndege zaongeza ndege zinazowasili Afrika kwa asilimia 13.3

    (GMT+08:00) 2017-10-12 09:59:49

    Njia mpya za safari za ndege na mustakabali mpya wa bara la Afrika vimechangio ongezeko la ndege za kimataifa zinazowasili barani Afrika kwa asilimia 13.3 katika kipindi cha mwanzo na cha kati cha mwaka 2017, ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo.

    Ripoti iliyotolewa na kampuni ya utalii ya kimataifa ForwardKeys kwenye mkutano wa mwaka 2017 wa safari za ndege wa Afrika unaofanyika Kigali, inaonyesha kuwa ongezeko hilo lilitokana na kuzinduliwa kwa njia 82 za safari za ndege, ambazo ongezeko la asilimia 17.8 linatoka Amerika, asilimia 12.7 kutoka Ulaya, asilimia 12.5 kutoka Afrika na asilimia 16.4 kutoka Asia na pasifiki.

    Ripoti pia inasema, idadi ya abiria wanaofika katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki imeongezeka kwa asilimia 12.2, wengi wa wasafiri wakiwa wanatoka Ulaya. Na wanaotoka Amerika, na Asia na Pasifiki ni wachache kuliko wanaosafiri kutoka sehemu za ndani za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako