• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la IS laanza tena mashambulizi ya kujilipua kufuatia operesheni za kijeshi zinazofanywa na jeshi la Syria

  (GMT+08:00) 2017-10-12 10:09:44

  Kundi la IS limefanya mashambulizi ya mabomu ya kujitoa mhanga mjini Damascus, ikiwa ni ishara ya kukata tamaa kwa wapiganaji wa kundi la IS kufuatia operesheni za kijeshi zinazofanywa na jeshi la Syria.

  Washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga walijaribu kujipenyeza katika kituo cha polisi kilichoko katikati mwa mji wa Damascus, lakini walishindwa kuingia kwenye kituo hicho baada ya kupambana na walinzi, na hivyo wawili kati yao walijipua karibu na kituo hicho. Mshambuliaji wa tatu alikimbilia kwenye soko moja la nguo na kujilipua, ambapo polisi wawili waliuawa na raia karibu kumi wa kawaida walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako