• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la UN lataka ratiba ya uchaguzi nchini DRC

    (GMT+08:00) 2017-10-12 10:10:18

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC itoe ratiba ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

    Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la usalama mwezi wa Oktoba Bw. Francois Delattre, amesema baraza hilo linatarajia ratiba ya uchaguzi na utekelezaji wa hatua za kujenga imani.

    Baraza hilo limekubaliana na ujumbe mpya kuhusu utekelezaji wa haraka na wa pande zote wa makubaliano yaliyofikiwa mwaka jana, ambayo ni muhimu kwa mchakato wa uchaguzi wa kuaminika, wa amani na wenye utulivu.

    Makubaliano hayo yamemruhusu rais wa sasa wa nchi hiyo Bw Joeseph Kabila ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2001 kuendelea kubaki madarakani baada ya muda wake kumalizika, kwa masharti kwamba uchaguzi unatakiwa kufanyika mwaka huu. Lakini hadi sasa inaonekana kuwa uchaguzi hauwezi kufanyika mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako