• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Maasai Mara yachaguliwa mbuga bora ya wanyama Afrika

  (GMT+08:00) 2017-10-12 18:41:57
   

  Kenya imejiweka tena kwa jicho la kimataifa baada ya mbuga ya wanyama pori ya maasai Mara kuchaguliwa mbuga bora barani Afrika.

  Katika tuzo za World travel za kila mwaka, mbuga hii ilipewa tuzo hiyo kwa utajiri wake kwenye wanyama pori na huduma za kitalii.

  Mara ilizishinda mbuga nyingine za wanyama kama vile Kruger National Park ya Afrika Kusini, Serengeti ya Tanzania, Kalahari ya Botswana, Kidepo ya Uganda na Etosha ya Namibia.

  Tuzo hizi za kila mwaka zimeandaliwa Kigali Rwanda mwaka huu na zilishuhudia pia Bodi ya utalii ya Kenya ilichaguliwa namba moja katika Afrika.

  Mkurugenzi mkuu wa world Travel Graham Coke amesema wametambua juhudi a utalii wa Kenya na mafanikio waliyoyapata katika miaka ya hivi karibuni

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako