• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Wavuvi elfu 7 Lamu kulipwa fidia na wasimamizi wa mradi wa Lapset

  (GMT+08:00) 2017-10-12 18:42:26

  Zaidi ya wavuvi elfu 7 waliolazimika kuondoka katika makaazi yao kwa ajili ya mrdai wa Lapset wa bandari ya Lamu watalipwa fidia.

  Mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya mradi huo wa Lapset Silvester Kasuku amesema majadiliano ya kulipwa kwao yanaendelea baina yao na serikali pamoja na washikadau wa mradi huo.

  Kasuku ameahidi kwamba kabla ya fidia hiyo, kwa sasa wavuvi hao watapewa vifaa vya kisasa vya uvuvi vitakaowawezesha kuvua maji makuu baada ya eneo la uvuvi kujengwa bandari.

  Eneo la mkanda linalokuwa na samaki wengi sasa litakuwa marufuku kufanywa uvuvi jambo ambalo lilileta utata wa wavuvi hao

  Mradi wa bandari la Lamu utagharimu shilingi trilioni 2.5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako