• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Uzinduzi wa daraja la Kilombero kufanyika karibuni

    (GMT+08:00) 2017-10-12 18:42:56

    Uzinduzi wa Daraja la Mto Kilombero mkoani Morogoro, utafanyika wakati wowote kuanzia sasa baada ya ujenzi kukamilika kwa asilimia 100.

    Uibukuzi na Mawasiliano,

    Changamoto ya kivuko waliyokuwa nayo wananchi wa Ulanga, Malinyi na Kilimbero, itakamilika kwa daraja hili itakuwa msaada mkubwa kwao.

    Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wa wilaya hizo wanaunganishwa vyema na wananchi wa wilaya nyingine za mikoa ya kusini.

    Moja ya changamoto inayoikabili Wilaya ya Ulanga ni kutounganishwa na wilaya nyingine kwa upande mikoa ya kusini, hali iliyofanya wilaya hiyo kuwa kama kisiwa, lakini pia kuna changamoto ya barabara kwa wilaya zote za Ulanga, Malinyi na Kilombero

    Naibu Waziri alisema kuwa changamoto hizo zitafanyiwa kazi haraka ili kuwasaidia wananchi. Wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi maarufu kwa kilimo cha mpunga na ufugaji, hivyo kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutasaidia usafirishaji wa mazao ya mpunga, ufuta, mahindi na mazao yatokayo na mifugo The

    Ikumbukwe kwamba mwaka jana mwezi Januari kivuko cha Mto Kilombero 'MV Kilombero ll' kilipinduka baada ya kusukumwa na upepo mkali ambapo watu 30 kati 31 waliokuwemo waliokolewa. Tukio hilo la kuzama kwa kivuko Mto Kilombero lilikuwa la pili baada ya mwaka 2003 pia kuzama na kuua watu kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako