• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Marekani atishia tena kusimamisha makubaliano ya biashara huria ya Amerika ya Kaskazini

  (GMT+08:00) 2017-10-12 18:45:37

  Rais Donald Trump wa Marekani ametishia tena kusimamisha makubaliano ya biashara huria ya Amerika ya Kaskazini yaliyosainiwa kati ya Marekani, Canada na Mexico, na kusema kuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya pande mbili na nchi hizo.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioongozwa na rais Trump na waziri mkuu wa Canada Bw. Justin Trudeau ambaye yuko ziarani nchini Marekani, rais Trump amesema mazungumzo ya kurekebisha makubaliano hayo ni magumu, na kama nchi hizo tatu hazitafikia maoni ya pamoja, makubaliano hayo yatasimamishwa.

  Kabla ya hapo, Rais Trump aliyakosoa makubaliano hayo mara kwa mara kwamba yamesababisha kupungua kwa nafasi za ajira kwenye sekta ya utengenezaji nchini humo, hata kutishia kujitoa kutoka makubaliano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako