• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajeshi nchini Kenya wawasaka wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kwenye maeneo ya pwani

  (GMT+08:00) 2017-10-12 18:47:22

  Msemaji wa jeshi la ulinzi la Kenya David Obonyo amesema jeshi la nchi hiyo limeongeza msako dhidi ya wapiganaji wa kundi la Al Shabaab walioingia nchini humo kutokea Somalia kwa lengo la kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya raia na vikosi vya usalama kwenye kaunti ya Lamu.

  Obonyo amesema, wapiganaji hao waliingia nchini humo kupitia msitu wa Boni ili kufanya mashambulizi zaidi katika Kaunti za Lamu na Garissa karibu na mpaka wa Kenya na Somalia. Jumatatu wiki hii, jeshi la ulinzi la Kenya KDF liliwaua wapiganaji watano wa Al Shabaab na kukamata bunduki aina ya AK-47 na risasi 321, mabomu matatu, na vifaa mbalimbali vya kulipuka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako