• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mzunguko mbaya wa hali ya peninsula ya Korea unatokana na uadui kati ya Korea Kaskazini na Marekani

  (GMT+08:00) 2017-10-12 19:03:55

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China bibi Hua Chunying amesema mzunguko mbaya wa hali ya peninsula ya Korea unatokana na uadui kati ya Korea Kaskazini na Marekani na kukosa kuaminiana na usalama.

  Habari zinasema waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Ri Yong-ho amesema nchi hiyo kamwe haitakubali kufanya mazungumzo kuhusu silaha za nyuklia, na kuitaka Marekani kuacha sera za kiadui dhidi ya nchi yake, pia amesema mapendekezo ya China na Russia pia hayakubaliki.

  Bibi Hua Chunying amesema mapendekezo ya China na Russia yalitokana na kujali ufuatiliani wa pande mbalimbali kwa uwiano, na yanasaidia kutatua matatizo ya sasa, hivyo pande husika zinatakiwa kufikiri kwa makini na kutoa majibu mazuri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako