• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Thamani ya huduma ya nguvukazi ya China yatarajia kufikia dola za Marekani trilioni 303.5 mwaka 2020

  (GMT+08:00) 2017-10-12 19:46:48

  Wizara ya nguvukazi na huduma za jamii ya China imesema, hadi kufikia mwaka 2020, thamani ya huduma ya nguvukazi ya China itafikia dola za Marekani trilioni 303.5.

  Ripoti ya mpango wa maendeleo ya huduma ya nguvukazi iliyotolewa na wizara hiyo imesema, katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya huduma ya nguvukazi nchini China inaendelezwa kwa kasi na imepata mafanikio makubwa. Mwishoni mwa mwaka jana, China ilikuwa na kampuni elfu 26.7 za huduma ya nguvukazi ambayo kipato chake kimefikia dola za Marekani trilioni 179.1. Ongezeko la mapato hayo limeendelea kuwa asilimia 20 katika miaka ya hivi karibuni.

  Wizara hiyo pia imesema, hadi kufikia mwaka 2020, watu laki 6 wanatarajiwa kufanya kazi katika sekta hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako