• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watalii wa kimataifa wanaokwenda Afrika yaongezeka kwa kasi

    (GMT+08:00) 2017-10-12 19:47:10

    Kampuni inayoshughulikia masuala ya utalii imesema, mpaka tarehe 20 Septemba, idadi ya watalii wa kimataifa waliokwenda Afrika imeongeza kwa asilimia 13.3 ikilingana na mwaka jana.

    Kampuni hiyo imetoa ripoti kwenye mkutano wa maendeleo ya usafiri wa anga wa Afrika uliofanyika mjini Kigali Rwanda. Ripoti hiyo pia imesema, tangu mwaka huu, njia 82 mpya za ndege za kimataifa zinazosafiri kwenda Afrika zimeanzishwa. Ongezeko la idadi ya watalii waliosafiri kwa ndege kutoka bara la Amerika ni asilimia 17.8, Ulaya ni asilimia 12.7, na Asia Pasifiki ni asilimia 16.4.

    Kampuni hiyo pia imesema, usafiri wa ndege wa Afrika unaendelezwa vizuri, na kama ukidumisha mwelekeo huo, usafiri wa ndege za moja kwa moja kati ya miji mbalimbali ya Afrika utakuwa rahisi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako