• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chelsea yaitoa Bayern Munich nje ya kombe la vilabu bingwa

  (GMT+08:00) 2017-10-13 08:37:29

  Wanawake wa Chelsea walinusurika dakika za mwisho chini Ujerumani na kufanikiwa kuwatoa Bayern Munich nje ya kombe la vilabu bingwa kupitia sheria ya mabao ya ugenini. Ikiongoza kwa bao 1-0 kutoka kipindi cha kwanza cha mechi, mshambuliaji wa Uingereza Fran Kirby alifunga bao kwenye dakika ya 60 na kuimarisha ari ya Chelsea.

  Bao hilo lilikiwacha kikosi cha Ujerumani kuhitaji mabao matatu lakini kikafanikiwa kupata mawili, kupitia Gemma Davison aliyejifunga na Lucie Vonkova aliyefunga wakiwa wamesaliwa na goli.

  Hatahivyo Chelsea ilifanikiwa na kuingia katika orodha ya timu 16 bora.

  Bayern ilidhani imefanikiwa dakika za lala salama wakati Simone Laudehr alipofunga mkwaju wa adhabu uliopigwa na Melanie Behringer lakini bao hilo likakataliwa kwa kudaiwa kumsukuma mwenzake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako