• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Aguero asema ni vigumu Messi kuihama Barcelona japokuwa pesa sio tatizo kwa klabu yake Man City

  (GMT+08:00) 2017-10-13 08:37:48

  Wakati mkataba wa mchezaji bora wa dunia anaekipiga katika timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi unaelekea ukingoni, nyota wa Man City, Sergio Aguero amesema ni vigumu kwa timu yake kumsajili mkali huyo wa soka. Aguero ambaye anacheza timu moja ya taifa na Messi amekiri kuwepo kwa ugumu wa kuinasa saini ya nyota huyo kwakuwa mchezaji huyo ni nembo ya klabu ya Barcelona.

  Aguero haamini kama kunatumaini la Messi kujiunga na City, hata kama fedha si tatizo kwa klabu yake. Aguero hakuwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina ambacho kimecheza wiki hii kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la dunia baada ya kupata ajali ya gari huko Amsterdam mwishoni mwa mwezi Septemba iliyomsababishia kuvunjika kwa mbavu zake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako