• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msuva azidi kufanya mambo Morocco

    (GMT+08:00) 2017-10-13 08:38:05

    Winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva juzi aliifungia timu yake, Difaa Hassan El - Jadida bao muhimu la ugenini ikifungwa 2-1 katika mchezo wa Kombe la Ligi Morocco na Chabab Rif Hoceima Uwanja wa Mimoun Al Arsi mjini Al Hoceima. Kwa bao hilo, Difaa Hassan El – Jadida watahitaji ushindi wa 1-0 tu nyumbani kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

    Huo ni mwendelezo wa mwanzo mzuri kwa Msuva tangu ahamie timu hiyo miezi miwili iliyopita kufuatia kucheza Tanzania kwa muda mrefu.

    Na hilo linakuwa bao lake la nane tangu amejiunga na timu hiyo na la pili kwenye mechi za mashindano, mengine sita akifunga kwenye mechi za kirafiki, zikiwemo za ziara ya Hispania. Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na DHJ Julai 28 mwaka huu, baada ya kucheza Yanga ya Tanzania tangu mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako