• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa ulinzi wa Somalia na mkuu wa jeshi la nchi hiyo wajiuzulu

  (GMT+08:00) 2017-10-13 10:34:15

  Waziri wa ulinzi wa Somalia Abdirashid Abdullahi Mohamed na mkuu wa jeshi la nchi hiyo Ahmed Mohamed Jimale wamejiuzulu jana. Waziri wa habari wa Somalia Abdirahman Omar Osman amethibitisha kujiuzulu kwao na kusema waziri wa ulinzi alijiuzulu kwa sababu binafisi, lakini hakudokeza sababu ya kujiuzulu kwa mkuu wa jeshi, miezi sita tu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo. Hata hivyo kujiuzulu kwao kumekuja baada ya shutuma kali kutolewa dhidi ya operesheni za kijeshi zilizofanywa na jeshi la Somalia kusini mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya raia 10, na mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni na Al-Shabaab dhidi ya kituo cha jeshi na kusababisha vifo vya askari wengi wa serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako