• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya Rugby Kenya: Kabras Sugar, Kenya Harlequins zatinga robo fainali

    (GMT+08:00) 2017-10-16 08:15:35
    Timu za Kabras Sugar na Kenya Harlequins zimekuwa timu za kwanza kuingia robo-fainali kuu ya makala ya mwaka 2017 uwanjani RFUEA, Jumamosi.

    Kabras imekata tiketi baada ya kuirarua Strathmore Leos 41-7 na MKU Thika 34-5 katika mechi za Kundi A.

    Harlequins yenyewe imefuzu baada ya kuichabanga MKU Thika 38-12 na Strathmore Leos 19-10. Strathmore na MKU Thika zimeaga mashindano hayo na kuteremka katika shindano la Challenge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako