• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalaani shambulizi la bomu lililoua takriban watu 276 nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2017-10-16 18:46:49

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lu Kang, amesema China inalaani vikali shambulizi la bomu lililotokea Mogadishu, Somalia na kusababisha vifo vya watu takriban 276 na wengine 300 kujeruhiwa.

    Amesema China inapinga vikali aina yoyote ya ugaidi na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Somalia katika kupambana na magaidi na kulinda usalama na utulivu wa nchi. Aidha amesema China iko tayari kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika, ikiwemo Somalia, ili kukabiliana pamoja na changamoto zinazotokana na ugaidi na kubeba jukumu la kiujenzi katika kuimarisha amani na usalama wa Afrika.

    Shambulizi la bomu lilitokea Jumamosi kwenye eneo la maduka baada ya gari lenye mabomu kulipuka karibu na lango la hoteli, na kuharibu eneo. Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed ametangaza siku tatu za maombolezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako