• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bei za juu za mafuta zina uwezekano wa kusukuma juu hali ya maisha

    (GMT+08:00) 2017-10-16 19:19:32

    Bei ya juu ya mafuta inauwezekano wa kusukuma juu gharama za maisha.

    Siku ya Jumamosi, Tume ya Udhibiti wa Nishati iliongeza bei ya petroli na Sh3.37 kwa lita wakati ile ya dizeli na mafuta ya taa ilipanda Sh1.85 na Sh1.82 kwa mtiririko huo.

    Mwezi uliopita, bei ya petroli ilipanda na Sh2.22 wakati dizeli na mafuta ya taa bei yake iliongezeka kwa kiasi kidogo.

    Gharama ya petroli, dizeli na mafuta taa iliongezeka kwa asilimia 7.42, 6.13 na 4.76 kati ya Agosti na Septemba.

    Kiwango cha mfumuko wa bei ya mwezi wa Oktoba inatarajia kuwa juu kuliko asilimia 6.9 iliyotabiriwa na wanauchumi.

    Lita moja ya mafuta ya petroli sasa inanunuliwa kwa Sh101.67 mjini Nairobi wakati ile ya dizeli na mafuta ya taa ni Sh88.71 na Sh66.18 katika utaratibu huo.

    Kisumu, bei ya rejareja ya petroli ni Sh103.64, dizeli Sh90.89 na mafuta ya taa Sh68.1.

    Bei ya Mafuta Mombasa bei yake ni nafuu kidogo, ambako lita moja ya mafuta ya petroli inauzwa kwa Sh98.39. Dizeli na mafuta taa zinanunliwa kwa Sh85.44 na Sh63.42 kwa lita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako