• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali yaahirisha mnada wa tanzanite

    (GMT+08:00) 2017-10-16 19:21:15

    SERIKALI imeahirisha mnada wa Madini ya Tanzanite uliokuwa ufanyike kuanzia Oktoba 12 hadi 15, mwaka huu katika mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

    Wizara ya Madini imetoa taarifa kwa umma kuwa Mnada wa Madini ya Tanzanite umeahirishwa hadi hapo utakapotangazwa tena.

    Imekutokana wadau wa mnada wameomba kupatiwa muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa wingi na kwamba uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Mirerani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako