• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mke wa rais wa Sierra Leone ashirikiana na shirika la China kutoa maziwa ya unga kwa watoto wa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2017-10-16 20:14:28

    Mke wa rais wa Sierra Leone Bibi Sia Nyama Koroma akishirikiana na Shirika la utengenezaji wa bidhaa za watoto la China Beingmate wamekabidhi maziwa ya unga ili kuwapatia virutubisho watoto zaidi ya elfu 20 wenye umri wa mwaka 1 hadi miaka 5 na mama wanaonyonyesha wa huko.

    Katika hafla ya kukabidhi maziwa hayo, Bibi Koroma amesema, kazi yake ya kwanza ni kushiriki kwenye shughuli ya kupunguza kiwango cha vifo vya wanawake barani Afrika. Ameeleza kuwa virutubisho vina umuhimu mkubwa kwa wanawake na watoto, hivyo maziwa ya unga yaliyotolewa na shirika la Beingmate yana maana kubwa kwa wanawake na watoto wa Afrika. Aidha kwa niaba ya rais Koroma na wanawake na watoto wa Sierra Leone, amelishukuru shirika la China, na kulitaka kutoa mchango katika shughuli ya afya ya wanawake na watoto kupitia juhudi za pamoja za pande mbili.

    Kwa upande wake balozi wa China nchini Sierra Leone Bw. Wu Peng amesema, makabidhiano hayo sio tu yanamaanisha undugu kati ya watu wa China na Sierra Leone, bali pia yameonesha kuwa mashirika ya China yanatimiza ahadi ya kutekeleza jukumu la kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako