• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Awamu ya kwanza ya tamasha la kimataifa la filamu za China na Afrika yafunguliwa nchini Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2017-10-17 18:53:47

  Awamu ya kwanza ya tamasha la kimataifa la filamu lza China na Afrika lilifunguliwa jana usiku huko Cape town nchini Afrika Kusini. Watu wa sekta ya filamu kutoka China, Afrika Kusini, Boswana, Tanzania, Ghana, Namibia na Nigeria wanakusanyika na kuonesha mafanikio ya sekta ya filamu na kubadilishana uzoefu wa utengenezaji wa filamu.

  Tamasha hilo linafanyika kwa siku tatu, na filamu nyingi za China na Afrika zitaoneshwa. Mwenyekiti wa kamati ya kuandaa tamasha hilo ambaye pia ni mkuu wa CRI Bw. Wang Gengnian alitoa salamu za pongezi kwa tamasha hilo akisema ingawa umbali kati ya China na Afrika ni mkubwa, lakini pande mbili zina hadithi nyingi za kuvutia. Amelitaka tamasha hilo litangaze utamaduni na hadithi za kuvutia za nchi hizo na watu wake kwa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako