• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kampuni ya sukari ya Mumias yarejelea tena oparesheni zake

    (GMT+08:00) 2017-10-17 19:15:19

    Kampuni ya sukari ya Mumias nchini Kenya imerejelea tena oparesheni zake baada ya kufungwa kwa miezi 8 kufanyika ukarabati mapema mwaka huu.

    Bali na ukarabati kampuni hiyo pia ilikuwa haipati miwa ya kutosha kutoka kwa wakulima.

    Mkuu wa halmashauri ya wakurugenzi Dtk. Kenneth Mulwa amesema kiwanda kilifunguliwa tena wikendi.

    Aidha amesema halmashauri hiyo imeweka usimamizi mpya Nashon Aseka akiwa mkurugenzi mkuu.

    Wakulima wa eneo hilo la Mumias sasa wametakiwa kupeleka miwa yao kwenye kiwanda hicho ili kusaida juhudi za kurejesha oparehsni kamili za uzalishaji wa sukari.

    Kampuni hiyo imekuwa ikikumbwa na matatizo ya kifedha na hadi sasa serikali imeipa shilingi bilioni 3.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako