• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliko Dangote aanzisha mpango wa kuwashirikisha wahitimu wa vyuo vikuu kulima mpunga

    (GMT+08:00) 2017-10-17 19:19:23

    Mfanyabiashara maarufu wa Nigeria Aliko Dangote ameanzisha mpango wa kuwashirikisha wahitimu wa vyuo vikuu kulima mpunga.

    Mpango huo unaotekelezwa na kampuni yake ya Dangote Rice Limited iliyojikita kwenye kilimo hicho,katika Jiji la Kogi nchini Nigeria, unalenga kupunguza uhaba wa ajira kwa wahitimu hao.

    Katika utekelezaji huo kampuni hiyo inawashirikisha wahitimu hao kulima hekta 100 kwa ahadi ya kununua mpunga utakaozalishwa huku yenyewe ikitoa mbegu, ushauri wa namna ya kukabiliana na changamoto za kilimo, viuatilifu na mbolea.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Dangote Rice, Devakumar Edwin alisema mradi huo ni sehemu ya kuwaandaa wajasiriamali watakaoleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji wa sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako