• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchujo wa kufuzu kombe la dunia: Italia yapewa Sweden

    (GMT+08:00) 2017-10-18 08:47:27
    Timu ya taifa ya Italia itamenyana na Sweden katika mchezo wa mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia mwakani nchini Urusi

    Katika droo maalum iliyopangwa mjini Zurich, Uswisi yalipo makao makuu ya Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), Ireland ya kaskazini itamenyana na Uswisi.

    Jamhuri ya Ireland yenyewe itamenyana na Denmark, wakati Croatia itamenyana na Ugiriki.

    Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 9 na 11 na za marudiano Novemba 12-14, mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako