• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali YA Kenya yafufua mipango ya ujenzi wa angatua ya pili itakayogharimu Sh37bn katika JKIA

    (GMT+08:00) 2017-10-18 19:14:06

    Serikali ya Kenya imefufua upya mipango ya ujenzi wa angatua ya pili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta itakayogharimu sh37 bilioni.

    Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini Kenya (KAA) jana ilisema serikali imetuma maombi ya ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa angatua ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

    Katika notisi kwenye vyombo vya habari jana,KAA imetoa nafasi kwa washauri kutuma maombi ya zabuni kwa ajili ya muundo wa mradi huo,usimamizi wa ujenzi,na mkandarasi wa mradi..

    Mshauri huyo aidha atahitajika kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa ndani ya bei ya mkandarasi na muda uliolengwa kwa ukamilishaji.

    Serikali imeamua kujenga angatua ya pili katika uwanja wa ndege ulio na shughuli nyingi katika ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kughairi mipango ya Sh50 bilioni ya mradi wa Greenfield Terminal Project kutokana na kile ilichosema ni kuongekezeka kwa uwezo katika kituo kilichokarabatiwa katika JKIA.

    Hata hivyo ujenzi wa angatua umechelewa kwa takriban miaka mine sasa kutokana na kile ambacho KAA inasema ni AfDB kuchelewa kutoa fedha.

    Mradi huu utakapokamilika ,angatua mpya inatarajiwa kuongeza mara mbili kiwango cha ndege katika uwanja huo kutoka 25 hadi 45 kwa saa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako