• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la Bakool la Somalia lapiga marufuku miraa

    (GMT+08:00) 2017-10-18 19:14:54

    Eneo la Bakool nchini Somalia limepiga marufuku matumizi ya miraa,na kuzua wasiwasi katika mnyororo wa uuzaji bidhaa hiyo.

    Wauzaji nje bidhaa hiyo wanahofia marufuku hiyo iliyotolewa na eneo la Bakool huenda ikasababisha mgogoro katika sekta hiyo.

    Bakool,eneo dogo la kusini magharibi mwa Somalia,hutumia tani moja ya miraa kwa siku.

    .Tani moja ni magunia kumi ya miraa yanayogharimu Sh50,000 na gharama za usafirishaji za $3,000 (takriban Sh300,000), ikimaanisha kuwa gharama za bidhaa hiyo inapofika Bakool ni Sh800,000 kwa tani kila siku .

    Mauzo ya miraa kwa wastani hubebwa na ndege 10 za mizigo zinazobeba tani 9 za bidhaa hiyo zenye gharama ya zaidi ya Sh63 milioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako