• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima Rwanda watia saini mkataba wa kuboresha uzalishaji viazi

    (GMT+08:00) 2017-10-18 19:15:20

    Wakulima nchini Rwanda wanasema mkataba mpya uliotiwa saini kati ya Kituo cha Kimataifa cha Viazi (CIP) na BlackPace Africa Group ili kuongeza uzalishaji wa viazi Afrika,ikiwa ni pamoja na Rwanda,ni jambo la busara ambalo litaboresha uzalishaji.

    Akizungumza kuhusu mkataba ambao umetiwa saini wiki iliyopita,Rais wa muungano wa wakulima wa viazi katika wilaya ya Nyabihu nchini Rwanda Jean Damascene Ntawushobora alisema wakulima wakulima wanataka viazi tofauti vinavyotoa mazao mengi ambavyo vinafaa katika aina tofauti za mchanga nchini kote.

    Alisema wanakuza aina za viazi ambazo zililetwa na kituo cha awali cha Kilimo wakati aina nyengine zimeagizwa kutoka nchi jirani kama vile Uganda na DR Congo.

    Aliongeza kuwa utafiti wowote ambao unalenga kuboresha aina za viazi unakaribishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako