• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Kenya amesema ni vigumu kuhakikisha uchaguzi wa kuaminika

  (GMT+08:00) 2017-10-19 09:00:47

  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Wafula Chebukati, amesema ni vigumu kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa Kenya uliopangwa kufanyika tarehe 26 Oktoba kuwa utakuwa huru na wa haki.

  Amesema hataki kuendelea kusukumwa na makamishna walio wengi wa tume ya uchaguzi akubali mapendekezo ya kisheria yenye maslahi ya vyama ambayo hayana msingi wa kikatiba.

  Amesema amejaribu mara kadhaa kufanya mabadiliko muhimu lakini mapendekezo yake yamepingwa na makamishna wa tume. Kwenye mazingira kama hayo, ni vigumu kuhakikisha kuwa uchaguzi utakuwa huru, wa haki na wa kuaminika.

  Bw Chebukati ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kamishna mmoja wa tume Bibi Rosely Akombe kujiuzulu na kuongeza hali ya sintofahamu kisiasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako