• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Ufaransa lapitisha sheria mpya ya kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-10-19 09:21:48

    Bunge la Ufaransa limepitisha mswada ulioongozwa na rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo kuhusu usalama wa taifa na mapambano dhidi ya ugaidi, ambao unatarajiwa kuchukua nafasi ya utekelezaji wa hali ya dharura utakaomalizika Novemba mosi.

    Baraza la seneti la Ufaransa limepiga kura 244 za ndio na nyingine 22 za hapana na kupitisha mswada uliotolewa na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo GĂ©rard Collomb.

    Kwa mujibu wa mswada huo mpya, serikali itapewa mamlaka ya kuwaweka kizuizini watu wanaotishia usalama wa umma, kupekua nyumba za washukiwa, kukagua magari katika maeneo muhimu na kufunga sehemu za kidini zinazoeneza itikadi kali.

    Habari zinasema mwaka huu Ufaransa imezuia majaribio 13 ya mashambulizi ya kigaidi dhidi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako