• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yarudisha watu 45 waliokuwa waasi wa DRC

    (GMT+08:00) 2017-10-19 09:43:27

    Uganda imewarudisha watu 45 waliokuwa waasi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kuwanyang'anya silaha na kuwasaidia kurudi katika jamii.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema, watu hao 45 waliokuwa wanachama wa kundi la M23 waliomba kurudi nyumbani kwa hiari.

    Watu hao walirudi kupita mji wa mpakani Bunagana na kukabidhiwa kwa balozi wa DRC nchini Uganda Bw Jean Pierre Massala.

    Serikali za Uganda, DRC na kundi la M23 walifikia makubaliano mwaka 2014 kuhusu kuwarudisha waasi 1,377 waliokuwa katika shule ya mafunzo ya kijeshi ya Bihanga, eneo la Ibanda, ili kuwanyang'anya silaha na kuwasaidia kurudi katika jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako