• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasisitiza ahadi ya kusimamisha mapambano daima

    (GMT+08:00) 2017-10-19 10:03:12

    Sudan Kusini imesisitiza tena ahadi yake ya kurejesha usitishaji vita wa kudumu baada ya kiongozi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa kukosekana kwa usalama nchini humo kunatokana na ukosefu wa nia ya kisiasa ya kusimamisha mapigano ya kijeshi.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo Bw. Mawien Makol amesema serikali ya Sudan Kusini itaendelea na juhudi za kutimiza ahadi ya kusimamisha mapambano daima wakati wa mazungumzo kati yake na maofisa wa ngazi ya juu wa Shirika la maendeleo la kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

    Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia ulinzi wa amani Bw. Jean-Pierre Lacroix amesema, serikali ya Sudan Kusini bado haijashiriki kikamilifu kwenye mchakato wa amani, ambao unadhaniwa kuwa ni fursa ya mwisho ya kukomesha mgogoro uliomudu kwa miaka minne nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako