• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethipoa:Benki kuu ya Ethiopia yashukisha thamani sarafu yake kwa asilimia 15

    (GMT+08:00) 2017-10-19 18:02:16

    Benki kuu ya Ethiopia imeshukisha thamani ya sarafu yake kwa asilimia 15 ili kuinua biashara ya bidhaa za nje.

    Dola moja ya Marekani sasa imeuzwa kwa 26.92 dhidi ya birr ya Ethiopia kutoka 23.41.

    Kwa mujibu wa Yohannes Ayalew gavana wa benki kuu ya Ethiopia,ni kwamba hatua hiyo inalenga kufungua fursa zaidi za biashara ya mauzo ya nje ya bidhaa iliyokwama katika mda wa miaka 5.

    Isitoshe benki ya dunia na shirika la kimataifa la fedha duniani wamekuwa wakisisitiza nchi ya Ethipia kufanya hivyo ili kuwa sawa na ushindani wa biashara na soko la kimataifa.

    Ethiopia inaongoza biashara ya kahawa barani Afrika lakini mapato yake yako chini kutokana na mauzo duni ya nje ya bidhaa.

    Mwaka jana Addis Ababa imepata dola bilioni 2.9 kutoka malengo la dola bilioni 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako