• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Ethiopia yawaonya wafanya biashara wanaopandisha bei ya bidhaa

    (GMT+08:00) 2017-10-19 19:11:18

    Serikali ya Ethiopia leo imewaonya wafanya biashara wanaojaribu kuumiza umma kwa kuongeza bei ya bidhaa zinazotoka nje baada ya kushuka kwa thamani ya sarafu.

    Kwa mujibu wa Mamlaka ya Biashara na Kuwalinda Wateja ya Ethiopia, baadhi ya wafanya biashara wanajaribu kuficha bidhaa, hususan zinazotoka nje, ili baadaye kuongeza bei kutokana na kiwango cha sasa cha birr ya Ethiopia ETB. Benki ya Taifa ya Ethiopia hivi karibuni ilitangaza mpango wa kushusha thamani ya birr ya Ethiopia kwa asilimia 15, ili kuleta ufanisi hadi kufikia Jumatano ya wiki iliyopita, hatua ambayo imelenga zaidi kufikia lengo la nchi la kuongeza mapato yake kutoka sekta ya uagizaji katika mwaka wa fedha wa 2017 na 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako