• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yaihimiza jumuiya ya kimataifa kuweka mazingira kwa mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-10-19 19:13:41

    Mwenyekiti wa kamati ya umoja wa majimbo ya Russia Bw. Valentina Matviyenko amesema, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuweka mazingira kwa ajili ya mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

    Akiongea kwenye ufungaji wa mkutano wa 137 wa muungano wa mabunge ya nchi mbalimbali, Bw, Matviyenko amesema, katika mkutano huo Russia imefanya mazungumzo na Korea Kaskazini na Korea Kusini kwa nyakati tofauti, na kupendekeza kuwa pande mbili zinatakiwa kufanya mazungumzo katika mkutano huo. Korea Kusini imesema inapenda kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini, lakini Korea Kaskazini imesema haijawa tayari kwa mazungumzo.

    Bw. Matviyenko amesema, kwa vile kuna hali ya kutoaminiana, kwa sasa hakuna mazingira kwa pande za Korea Kusini na Korea Kaskazini au Korea Kaskazini na Marekani kufanya mazungumzo. Russia itafanya juhudi zote kuhimiza pande mbalimbali kufanya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako