• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SimbaSC yamtangaza Masoud Djuma kuwa kocha mpya msaidizi

    (GMT+08:00) 2017-10-20 08:32:31

    Klabu ya Simba jana ilimtambulisha aliyekuwa kocha wa Rayon Sport ya Rwanda Masoud Djuma kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja ambaye juzi alitangaza kuachana na klabu hiyo. Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara alimtangaza Masoud Djuma kuchukua nafasi ya kocha msaidizi katika klabu yao hiyo ya Simba na kuwaomba wanachama na mashabiki wa Simba kumpa ushirikiano kocha huyo.

    Mbali na hilo Manara amekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kocha wao Mkuu Omog ameondoka klabuni hapo kwa sababu hajalipwa mshahara na kusema kuwa wao Simba hawajawahi kuwa na njaa na kusema kuwa kocha mkuu wao anaendelea na mazoezi na kikosi chao hivyo huo unaosambaa ni uzushi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako