• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Antonio Conte amuonya Mourinho kutofuatilia masuala ya Chelsea

  (GMT+08:00) 2017-10-20 08:34:28

  Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amemuambia kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwamba aangalie timu yake na aache kufuatilia masuala ya klabu ya Chelsea na kushangazwa na kitendo cha kocha huyo kuwafuatilia.

  Kauli ya Antonio Conte inakuja baada ya Jose Mourinho kudai kwamba kuna makocha ambao wachezaji wao wakipata maejeraha huwa wanapiga sana kelele kauli ambayo ilionekana kama kijembe cha moja kwa moja kwa Conte. Chelsea imeambulia alama moja tu katika michezo yao mitatu iliyopita katika msimu huu na Jumamosi hii wataikabili Watford huku Ngolo Kante, Victor Moses, Tiomoue Bakayoko na David Luiz wakiwa mashakani kuukosa mchezo huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako