• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wiki ya kuhimiza uzalishaji usiosababisha uchafuzi yahimiza kutumia fursa zilizopo barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-10-20 08:57:42

    Watunga sera na wataalamu waliokusanyika mjini Addis Ababa Ethiopia kwenye maadhimisho ya wiki ya kuhimiza ongezeko la uchumi bila kuchafua mazingira, wamesisitiza umuhimu kwa Afrika kutumia fursa ambazo hazijatumika za kuhimiza ongezeko la uchumi bila uchafuzi.

    Maadhimisho hayo yamewakutanisha maofisa 500 wakiwa ni mawaziri, wawekezaji na watunga sera, kuhimiza kutafuta mbinu za kuleta mageuzi ya kuhimiza ongezeko la uchumi bila kusababisha uchafuzi.

    Washiriki wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya miradi kwenye nchi zinazoendelea, na usimamizi mzuri wa raslimali ili kushughulikia changamoto za usalama wa maji na chakula.

    Naibu waziri mkuu wa Ethiopia Bw Demeke Mekonnen ameitaka jumuiya ya kimataifa kuhimiza juhudi za kufanya maendeleo yasiyosababisha uchafuzi wa mazingira barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako