• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kuu ya Iraq yazuia nchi za nje kufanya biashara ya mafuta na jimbo la wakurdi

    (GMT+08:00) 2017-10-20 09:30:58

    Wizara ya mafuta ya Iraq imesema serikali za nchi za nje na mashirika ya mafuta ya nje hayaruhusiwi kufanya biashara ya mafuta na jimbo la wakurdi bila idhini ya serikali kuu ya Iraq.

    Waziri wa mafuta ya Iraq Bw Jabbar Luaiby ametoa taarifa akisema kwa mujibu wa katiba na sheria, ni serikali kuu ya Iraq na wizara yake ya mafuta tu zina mamlaka ya kusaini makubaliano na nchi za nje kuhusu uwekezaji na uchimbaji katika sekta ya mafuta na gesi nchini humo, na makubaliano yoyote yaliyosainiwa bila ruhusa ya serikali kuu ya Iraq yamekuwa batili.

    Wakati huo huo mamlaka ya sheria ya Iraq imetoa hati ya kukamatwa kwa naibu mwenyekiti wa jimbo ka wakurdi Bw Khoslat Rasool, kutokana na kauli yake ya kuliita jeshi la serikali ya Iraq lililoingia katika jimbo la wakurdi kuwa "jeshi la uvamizi".

    Msemaji wa kamati ya juu ya sheria ya Iraq Bw Abdul Sattar amesema mahakama ya Baghdad imetoa hati ya kukamatwa kwa Bw. Rasool kutokana na kauli yake dhidi ya jeshi la serikali ya Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako