• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Ulaya watarajia mazungumzo ya Brexit yapate maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-10-20 10:00:17

    Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya umefunguliwa katika makao makuu ya umoja huo mjini Brussels, ambapo viongozi wengi wa nchi wanachama wa umoja huo wameeleza matarajio yao kuwa waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May atalegeza zaidi msimamo wake ili kukwamua mazungumzo yaliyokwama kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

    Bibi May pia anatarajia matokeo mazuri yatapatikana kwenye mazungumzo ya Brexit. Amesema Uingereza na Umoja wa Ulaya zinapaswa kuzingatia maendeleo yaliyopatikana kwenye mazungumzo hayo, na kutoa mipango ya kutia hamasa katika wiki kadhaa zijazo.

    Habari zinasema mkutano huo wa Umoja wa Ulaya ni muhimu kwa mazungumzo ya Brexit, na pande mbili zinatarajia kuwa mkutano huo utaweza kutoa msukumo mpya kwa mazungumzo ya Brexit.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako