• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping ahamasisha wananchi kuuhimiza ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya upate maendeleo mapya

    (GMT+08:00) 2017-10-20 10:16:43

    Katibu mkuu wa Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Xi Jinping aliposhiriki katika mjadala na wajumbe kutoka mkoa wa Guizhou walioko Beijing kuhudhuria Mkutano mkuu wa 19 wa CPC, amesema ripoti ya Mkutano mkuu huo imeweka bayana mwelekeo wa maendeleo kwa chama na nchi katika siku zijazo, ambayo ni ilani ya kisiasa na mwongozo wa utendaji wa Chama cha Kikomunisti cha China unaoongoza wananchi wa makabila mbalimbali kote nchini kushikilia na kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya. Amesema inatakiwa kujifunza na kuelewa vizuri fikra mpya ya ujamaa wenye umaalumu wa China unapoingia katika zama mpya, kujifunza na kuelewa vizuri umaalumu mpya wa mabadiliko ya migongano mikuu iliyopo katika jamii ya China, kujifunza na kuelewa vizuri malengo mapya ya kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya ujamaa kwa vipindi viwili, kujifunza na kuelewa vizuri matakwa mapya ya ujenzi wa chama. Bw. Xi amewataka wananchi wote washikamane na kufanya juhudi kwa pamoja ili kusukuma mbele Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako