• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya ukaguzi wa mahesabu ya Iran yasema Ahmadinejad anatakiwa kuwajibika na hasara ya mali ya taifa

    (GMT+08:00) 2017-10-20 18:46:21

    Mahakama kuu ya ukaguzi wa mahesabu ya Iran imesema, rais wa zama wa nchi hiyo Bw. Mahmoud Ahmadinejad anatakiwa kuwajibika na hasara ya dola bilioni 1.1 za kimarekani katika mali za taifa katika muda wake wa kazi. Hasara hiyo inahusiana na kosa la uamuzi lililofanywa na Bw. Ahmedinejad kuhusu biashara husika ya kampuni ya taifa ya mafuta katika muda wake wa pili wa urais.

    Mahakama imetoa ripoti ikisema, kutoka mwaka 2008 hadi 2012, kampuni hiyo ilinunua dizeli kutoka nchi za nje bila ya kupata kibali cha idara husika, na katika hali ambayo mafuta hayo yalizidi mahataji halisi ya nchi hiyo. Mbali na hayo kampuni hiyo ilishindwa kupata malipo baada ya kuuza mafuta kwa wateja wa ndani. Fedha hizo zilitakiwa kuhesabiwa mwaka 2008, lakini serikali ya Ahmadinejad haikufanya hivyo, na kusababisha hasara kubwa kwa nchi hiyo.

    Lakini ripoti hiyo haijataja jinsi Bw. Ahmadinejad atakavyowajibika na hasara hiyo .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako