• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wahimiza kupunguza kiwango cha vifo vya watoto

    (GMT+08:00) 2017-10-20 18:46:45

    Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ikisema, ingawa idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliofariki kote duniani imekuwa chini zaidi katika historia, lakini kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeongezeka kutoka asilimia 41 ya mwaka 2000 hadi asilimia 46 ya mwaka 2016.

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Shirika la Afya Duniani WHO, Benki ya Dunia na Ofisi ya idadi ya watu ya Idara ya Mambo ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja wa Mataifa zimetoa ripoti ya pamoja kuhusu "Mwelekeo na Kiwango cha vifo vya Watoto kwa Mwaka 2017". Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana watoto elfu 15 wenye umri chini ya miaka mitano walifariki kila siku kote duniani, wakiwemo watoto elfu 7 wachanga waliofariki ndani ya siku 28 baada ya kuzaliwa.

    Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa, watoto wengi wachanga waliofariki walitokea katika eneo la Asia ya Kusini na sehemu ya Afrika kusini mwa Sahara, ambao ni zaidi ya asilimia 75.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako