• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yazalisha tani 74.6 za dhahabu katika miezi 9 ya mwanzo ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-10-20 18:47:04

    Wizara ya madini ya Sudan imetoa ripoti ikisema, katika miezi 9 ya mwanzo ya mwaka huu uzalishaji wa dhahabu wa nchi hiyo umefika tani 74.6.

    Ripoti hiyo imesema kampuni za madini za jadi za Sudan zimezalisha tani 63.2 za dhahabu, ambazo ni maradufu ya mpango. Serikali ya nchi hiyo inapanga kupanua utafutaji wa madini ya dhahabu mwaka kesho, ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu.

    Serikali ya Sudan inachukua hatua mbalimbali kuinua uzalishaji wa dhahabu wa nchi hiyo, ili kuifanya Sudan iwe moja ya nchi zinazozalisha dhahabu kwa wingi duniani. Wachambuzi wanaona kufuatia ongezeko la uwekezaji wa kigeni, uzalishaji wa dhahabu unakadiriwa kuongezeka ndani ya muda mfupi.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia, Sudan inachukua nafasi ya tatu katika nchi za Afrika zinazozalisha dhahabu kwa wingi, ikizifuata Afrika Kusini na Ghana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako