• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viwanda vya kutengeneza nguo vyatakiwa kukumbatia fursa mpya Afrika mashariki

    (GMT+08:00) 2017-10-20 19:55:07

    Viwanda vya kutengeneza nguo katika kanda nzima ya Afrika mashariki vimetakiwa kuanza kukumbatia technolojia mpya ya utengenezaji nguo ili kutosheleza mahitaji ya soko katika kanda hii. Mkurugenzi mkuu wa baraza la wafanya biashara Afrika mashariki Bi. Lilian Awinja amesema viwanda vya Afrika mashariki vinatakiwa kuanza kujifunza njia rahisi ya kutengeneza nguo kwa wingi wakati huu ambapo nchi za jumuiya ya Afrika mashariki zinapanga kuanza kutekeleza marufuku ya nguo za mitumba katika eneo hilo. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Umoja wa Afrika umekuwa ukitoa msukumo kwa nchi wanachama kukumbatia uchumi wa kiviwanda kama moja ya njia za kukuza kwa haraka uchumi wa nchi zao.Awinja alikuwa akisema hayo mjini Dar es Salaam siku chache tu kabla ya maonesho ya kibiashara ya Afrika mashariki yatakayofanyika Dar es salaam nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako