• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Oman kupiga jeki sekta ya utalii Zanzibar

    (GMT+08:00) 2017-10-20 19:55:29

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema ujumbe wa viongozi wa Serikali ya Oman nchini Tanzania ulilenga kuimarisha masuala ya uchumi na maendeleo na kuitangaza sekta ya utalii nchini humo.Akizungumzia ziara hiyo, waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud Mohammed amesema mafanikio mengi yalipatikana kwenye ziara hiyo ikiwemo serikali ya Oman kukubali kulifanyia ukarabati mkubwa Jengo la Bait-al-Jaib lililopo Mji Mkongwe wa Zanzibar na kulirudisha katika hadhi yake ya asili kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii. Amesema Oman ipo tayari kugharamia ujenzi huo na kinachosubiriwa ni kupitiwa michoro ya ujenzi wa jengo na Kitengo cha miji ya Kale kilichoko urithi wa kimataifa ambacho ujumbe wake uko Zanzibar.Waziri huyo pia amesema serikali ya Oman imekubali kusaidia kazi za utafiti wa nishati na mafuta kutokana na kuwepo kwa taarifa za Zanzibar kuwa na dalili za kupatikana kwa mafuta.Ujumbe huo wa Oman ulioongozwa na waziri wa Mafuta na Gesi Bw. Mohamed Hamad Al-Rumhy ulipata nafasi ya kuzungumza na rais John Pombe Magufuli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako