• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo vimeongezeka hadi kufikia 71 katika mashambulizi ya misikiti miwili nchini Afghan

    (GMT+08:00) 2017-10-21 18:17:38

    Watu 71 wameuawa na wengine 83 kujeruhiwa wakati milipuko miwili ya kujitoa mhanga kutokea Ijumaa jioni kwenye misikiti miwili katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul na mkoa wa magharibi wa Ghor.

    Jumla ya watu 41 waliokuwa wakifanya ibada waliuawa na wengine 61 kujeruhiwa baada ya mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga kutokea kwenye msikiti wa Imam-e-Zaman huko Dasht-e-Barchi magharibi mwa Kabul.

    Msimamizi wa mambo ya utamaduni katika msikiti huo Bwana Najibullah Farhan amesema, watu 29 waliuawa ndani ya msikiti na wengine 12 wamefariki njiani walipopelekwa hospitali kwa matibabu.

    Wakati huo huo, watu 30 ikiwa ni pamoja na Fazl Ahmad Khan, kamanda mkuu wa kundi la kijeshi linalounga mkono serikali wameuawa na wengine 22 walijeruhiwa wakati mshambuliaji alipolipua msikiti katika kijiji cha Khoja Gan, wilaya ya Dulina jimbo la magharibi la Ghor.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako