• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yakosoa kitendo cha Marekani cha kuweka mfumo wa kukinga makombora

    (GMT+08:00) 2017-10-21 18:18:23

    Waziri wa mambo ya nje ya Russia Bw. Sergei Lavrov alipohudhuria mkutano wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia mjini Moscow, amesema Marekani na wenzi wake wa Ulaya na Asia Pasifiki ziliweka mfumo wa kukinga makombora, kitendo ambacho kinaharibu utulivu wa kimkakati wa kimataifa.

    Lavrov amesema, mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia ni muhimili wa mfumo wa usalama wa kimataifa wa kisasa, lakini mkataba huo unakabiliwa na changamoto kwamba baadhi ya nchi zinashuku vigezo na kanuni za mkataba huo, na baadhi ya nchi zinajaribu kutafuta maslahi kwa kutumia mkataba huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako