• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikundi cha polisi chashambuliwa magharibi mwa Misri

    (GMT+08:00) 2017-10-21 18:46:23

    Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imetoa taarifa ikisema kikundi kimoja cha polisi kimeshambuliwa jana na magaidi jangwani, na kusababisha vifo na majeruhi ya polisi wengi.

    Jana asubuhi kikundi cha polisi kilipokwenda eneo la Wahat el Bahariya lililoko kilomita 300 kusini magharibi ya mji mkuu Cairo ili kutafuta kituo cha magaidi, kilishambuliwa na magaidi njiani. Taarifa hiyo haidokezi idadi ya vifo na majeruhi.

    Habari kutoka idara ya matibabu ya huko zimesema polisi wasiopungua 35 wameuawa kwenye shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako