• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yaunga mkono mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-10-22 18:38:09

    Jumuiya ya kimataifa imesema inaunga mkono mapambano dhidi ya ugaidi baada ya mapigano makali kati ya polisi na magaidi yaliyotokea Ijumaa jangwani katika jimbo la Giza, nchini Misri kusababisha vifo vya polisi 16.

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limezihimiza nchi zote kushirikiana kikamilifu na serikali ya Misri na mamlaka husika katika suala la ugaidi.

    Katibu mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Ahmed Aboul-Gheit amelaani shambulio hilo na kuahidi kuiunga mkono Misri kupambana na ugaidi.

    Naye waziri wa vyombo vya habari wa Jordan, Mohammad Momani ameeleza kuwa Jordan inaiunga mkono juhudi ya Misri katika kupambana na magaidi na kulinda usalama na utulivu wa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako