• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chuo kikuu cha kijeshi nchini Afghanistan chashambuliwa na kusababisha vifo vya watu 15

    (GMT+08:00) 2017-10-22 18:52:19

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imetoa taarifa ikisema Chuo kikuu cha kijeshi mjini Kabul kimeshambuliwa jana na kusababisha vifo vya wanafunzi 15 na wengine wanne kujeruhiwa.

    Taarifa hiyo inasema saa 9 jana alasiri, mshambuliaji wa kujitoa muhanga alilipua bomu kando ya gari la wanafunzi wa chuo hicho, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu walioko ndani na kando ya gari hilo.

    Ikulu ya Afghanistan imetoa taarifa ikilaani vikali shambulizi hilo.

    Kundi la Taliban limedai kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako